PICHA: Wakimbizi katika kambi ya Sessi, Moyale Kenya
MARSABIT 15-03-2018
Zaidi ya kimama 500 kati ya wakambizi 8500 walioingia katika kaunti ndogo ya moyale kutoka nchini Ethiopia ni wajawazito kuligana na ripoti iliyotolewa na mashirika yasio ya kiserikali hapa jimboni yakishirikana na shirika la msalaba mwekundu nchini.
Wakimbizi hao waliwasili Moyale siku ya Jumamosi baada ya serikali ya Ethiopia kutekeleza mashambulizi dhidi ya jamii ya oromo ambayo inajumuisha makabila ya wengi nchini humo.
Wakimbizi hao pia waliingia mpakani moyale wakiwa wameandamana na mifugo wao huku ripoti zikisema kuwa zaidi ya Ngamia 600, Ngombe 2852, Mbuzi na Kondoo 700,Punda 55 na Mbwa 14 pia wameingia humu nchini.
Zaidi ya wakimbizi 70 walifika moyale wakiwa na majeraha, huku kukiripotiwa kwamba watu 16 walikuwa wameuwawa na majeshi ya serikali.
Kwa sasa hali ya taharuki imetanda katika mipaka ya Kenya na Ethiopia, huku wakimbizi wakiendelea kumiminika kwa wingi na kusababisha hofu ya kuzuka kwa maradhi ya kipindu pindu.
Serikali ya Kaunti ya Marsabit ikishirikana na mashirika ya misaada, imesema kuwa itaendelea kuwasaidia wakimbizi hao kwa kuwapa misaada ya chakula,malezi na huduma za afya.
Facebook: Radio Jangwani News Today
Twitter: Jangwani 106
Website: www.radiojangwani.co.ke

©RADIO JANGWANI 2018