PICHA:(MARIO KURAKI) MTOTO HUYU ANATOKA JAMII YA DAASNACH,KAUNTI YA MARSABIT.

Zaidi ya familia 4,600 zilizo na watoto yatima hapa Marsabit zitanufaika na mpango wa msaada kutoka kwa serikali.

Mratibu wa maswala ya watoto hapa Marsabit Simon Nyabuto Ogao amesema hilo litawezeshwa kufuatia kutolewa kwa zaidi ya shilingi milioni 5.5 na serikali ya kitaifa.
Amesema tayari shilingi milioni 3.3 ziko tayari kusambazwa wiki hii kwa watakaonufaika.
Kiasi fulani cha pesa hizo zitatumika kama ruzuku kuwafaidi wanafunzi yatima.
Wanafunzi wa bweni wametengewa shilingi 30,000 kila mmoja huku wale wa kutwa wakitarajiwa kunufaika na shilingi elfu 15 kwa kila mwanafunzi.

Ogao ameema haya hivi leo wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya mtoto mwafrika yaliyoandaliwa katika shule ya msingi ya Manyatta Jillo viungani mwa mji huu wa Marsabit.