PICHA: Kisima cha maji ilioko eneo la Arapal, Kaunti ya Marsabit.

KAUNTI YA MARSABIT 01-02-2018: Hali ya taharuki imetanda eneo la Arapal(Mt.Kulal) eneo bunge la Laisamis baada ya wavamizi kushambulia kijiji cha Arapal usiku wa kuamukia leo.
Kuligana na ripoti kutoka eneo hilo wavamizi hawa walianza mashambuzi saa nane usiku hadi saa kumi asubuhi.

Inadaiwa kuwa makazi ya wenyeji wa kijiji hicho yalishambuliwa kwa risasi na wavamizi hao na kusababisha hasara kubwa kama vile vyumba vya kitamaduni kuharibiwa.
Hata hiyo tunaarifiwa kuwa hakuna aliyejeruhiwa wala hakuna mifugo iliyochukuliwa katika mashambulizi hilo ambao linaaminiwa kutekelezwa kwa njama ya kulipa kisasa.
Shule ya msingi ya Arapal sasa imefungwa kwa muda baada ya wavamizi hao kushambulia kijiji hicho huku wenyeji wakitorikea usalama wao.

Maafisa wa polisi wakisaidiana na polisi wa akiba KPR sasa wametumwa eneo hilo ili kuwasaka wavamizi hao.
Mzozo huo inatokana na uhaba was lishe na maji kwa mifungo hasa wakati huu ambao kiangazi inashuhudiwa kaskazini mwa nchi.
Shambulio hilo linakuja siku chache baadaya wavamizi kuwauwa watu wawili akiwemo polisi wa akiba KPR na raia katika kijiji cha Chari Ashe katika wadi ya North Horr eneo bunge la North Horr.