Picha: Kaimu kaminshna wa Marsabit Samuel Gichohi amemkabidhi mmoja wa wanaoishi na ulemavu cherehani.
Wakaazi hapa jimboni wanaoishi na ulemavu sasa wana kila sababu ya kutabasamu baada ya wakfu wa kitaifa ya watu wanaoishi na ulemavu nchini kupeana vifaa vya matumizi kwao.

Akiongea nje ya afisi za kamishana wa jimbo hili wakati wa kupokeza vifaa hivyo,mwenyekiti wa kamati anayesimamia maswala ya misaada kwenye wakfu huo Prof Julia Ojiambo,amewataka wanaoishi na ulemavu jimboni kutumia vifaa hivyo kujiimarisha kimaisha ikiwa ni pamoja na kuendeleza bishara zao.

Aidha,amewaonya dhidi ya kuuza vifaa hivyo ambavyo anasema kuwa,iwapo zitatumika ipasavyo,huenda ,Maisha ya mamia yao ikaimarika.

Aidha,amewataka kubuni vikundi vya kibiashara na kuomba zabuni kutoka serikali ya kaunti kando na ile ya kitaifa.