Wahudumu wa bodaboda waliokamatwa hapo jana wakati wa maandamano wamefikishwa katika mahakama ya Marsabit hii leo na kushtakiwa kwa kosa la kushiriki maandamano bila idhini kwa nia ya kutatiza shughuli mjini.

Hata hivyo sita hao mbele ya mahakama wamekanusha shtaka hilo.

Sita hao ni Ibrahim Roba Gedo, Dida Lesuran Lechipan, Godfrey Karote Kimati, Mohamed Hassan Guyo,Yattani Alex Lunguyayo na Ibrahim Salesa Kombola ambao wameshtakiwa kwa kosa hilo pamoja na wenzao ambao hawakufika mahakamani.

Hakimu mkaazi wa mahakama ya Marsabit B.M Ombewa amewaachilia kwa dhamana ya shilingi elfu moja kila mmoja.

Kesi yao itasikilizwa tarehe 5 Januari, 2018 mwaka ujao.