PICHA: Vyoo vya umma vya kwanza kabisa kufunguliwa kaunti ya Marsabit.
TAREHE 10/08/2018-Ni afueni kwa wenyeji wa kaunti ya Marsabit baada ya serikali ya kaunti ikiongozwa na Gavana Mohamud Ali kufungua vyoo vitatu vya umma katika eneo bunge la Saku.
Vyoo hivyo ni vya kwanza kuwahi kufunguliwa na kaunti ya Marsabit,na vinatarajiwa kuwasaidia wafanyibiashara wanaotoka sehemu mbalimbali za kaunti hii kwa shughli zao za mchana.
Akizungumza na kituo hiki, msimamizi wa kundi la vijana liitwalo Ino, Ibrahim amesema kuwa kila atayetumia vyoo hivyo atatozwa ada ya shilingi ishirini, hela ambayo itatumika kufadhili shughli tofauti za vijana katika kaunti.
Baadhi ya wenyeji wameelezea furaha yao huku wakisimulia changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo kabla ya kufunguliwa kwa vyoo hivyo.
Walieleza kuwa walikuwa wakienda hotelini kwa kujisaidia na wakati mwingine wamiliki wa hoteli hizo huwanyima fursa ya kuingia.
Akihutubu katika uwanja wa Moi Girls Marsabit pindi baada ya kufungua rasmi vyoo hivyo, Gavana Ali ameahidi kuwa atapanga mikakati zaidi ili kuinua maisha ya vijana katika kaunti kwa kubuni nafasi zaidi za ajira na kuboresha sekta ya elimu.