dsc_0079
Tume ya kupambana na ufisadi nchini EACC hii leo imezindua rasmi siku ya kupigana na ufisadi duniani katika kaunti ya Marsabit.
“Kauli mbiu ya mwaka huu ni vita dhidi ya ufisadi ni jumu letu sote”
Warsha hii imewaleta pamoja viongozi kutoka serikali ya kaunti na kitaifa ili kutoa mafunzo kwa umma kuhusu jinamizi la ufisadi.

Baada ya uzinduzi huu mafisaa hawa kutoka tume ya EACC watakutana na viongozi wa serikali ya kaunti na wananchi na kuzungumza kuhusu ufisadi na jinsi ya kupiga vita.
Sherehe hii itafika kilele siku ya ijumaa ambao wananchi pamoja na viongozi watakusanyika katika uwanja wa mchezo wa Marsabit.
Naibu Gavana wa Kaunti ya Marsabit Omar Abdi alizindua sherehe hiyo ya kupiga vita ufisadi katika afisi ya kaunti.
Omar alisema kuwa ufisadi ni adui ya maendeleo tunastahili kupiga vita pamoja hadi kushinda.
Naye Mkurugenzi wa tume hiyo Ignius Wekesa alisema kuwa maafisa wake wataendeleza elimu kwa viongozi na wakaazi wa kaunti hii ya Marsabit.
Katika Hotuba yake wekesa alisisitisa kuwa vita dhidi ya ufisadi na jukumu letu zote.