dsc_0223
Shirika la Umoja wa kimataifa na maendeleo imetenga siku ya leo kuwa siku ya kuthamini takwimu muhumu ya bara la Africa.
Maadhimisho haya hufanyika kila mwaka katika mataifa ya bara Afrika.
Maadhimisho haya yamefanyika kaunti zote 47.
Shirika la kuthatimini takwimu nchi KNBS limeandaa sherehe ya maadhimisho katika Ukumbi wa St.Stephen hapa mjini Marsabit.
Hafla hiyo imewaleta pamoja wananchi,viongozi wanaowakilisha serikali kuu na kaunti na mashirika yasiokuwa ya serikali.
Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia ishirini na sita ya wanawake wajawazito wanajifungua katika vituo vya afya kinyume na hapo awali ishara kwamba sekta ya afya imekuwa bora zaidi.
Asilimia sitini na saba ya watoto walioko katika miezi 12-13 wanapata hitajika sawa na watoto asilimia sitini na nane kote nchini.
Upangaji uzazi ni changamoto kwa wakaazi wa Marsabit.
Takwimu zinaeonyesha kuwa asilimia kumi na moja ya familia wanapanga uzazi ikilinganishwa na asili mia hamisini na tatu nchini.
dsc_0225
Kamshina wa Kaunti ya Marsabit Magu Muthindika alihuturia sherehe hiyo na kusema takwimu ni muhimu kwani serikali inatumia kupanga miradi ya maendeleo.