PICHA: Maafisa wa Idara ya KWS na shirika LA NRT wakikagua gwaride, Mji wa Marsabit, Kenya.
TAREHE 31/07/2018
Maafisa wa shirika la huduma kwa wanyamapori nchini KWS wakishirikiana na shirika lisilokuwa la serikali la Northern Rangelanda Trust (NRT) hii leo wameandaa sherehe ya maadhimisho ya siku ya maafisa wanaolinda wanyama pori na mazingira nchini maarufu kama rangers.

Sherehe hiyo imewaleta maafisa hao pamoja ambapo walikagua gwaride la heshima kama njia ya kusherehekea ufanisi kwenye kazi zao za kulinda wanyamapori na mazingira.
Akizungumza katika hafla hiyo mkurungezi wa idara ya KWS hapa jimboni Obrien Lenguro amewaomba wenyeji wa kaunti hii kushirikiana na idara ya KWS na mashirika kama NRT kufanikisha azma ya kulinda wanyamapori na mazingira kwa ujumla.
“Mazingira ni maisha yetu lazima tuitunze na hii ndio wajibu wetu kama maafisa kutoka idara hizo hivyo basi askari wetu wamejitolea bila uonga” Asema Rubani O’Brien Lenguro.
Lenguro amesifia utendakazi nzuri wa maafisa hao wa kulinda wanyama pori akisema umesaidia pakubwa kupunguza visa vya uwindaji haramu jimboni.

Aidha, maafisa hao wamesherekea siku hii kwa kufanya usafi katika maeneo kadhaa katika mji huu Marsabit.
Afisa mtendaji wa shirika la NRT Titus Letapo pia amesifia utendakazi wa maafisa hao kwenye ufadhi wa mazingira na wanyamapori.
Letapo amepongeza pakubwa juhudi za maafisa hao za kuwakabili wawindaji haramu kwa kuweka maisha yao hatarini.
Ametoa wito kwa wenyeji wa jimbo hili kukumbatia wito wa uhifadhi wa mazingira.
Kila tarehe 31 mwezi julai ulimwengu husherehekea siku hii kama ukumbusho wa maafisa hao waliouawa au waliojeruhiwa wakiwa kazini, kando na kusherehekea kazi nzuri maafisa hao hujihusisha nayo ya kulinda mali asili na urithi wa kitamduni yaani mazingira.