Photo; Sadia Araru,Nominated MCA Moyale.
Mwakilishi mteule wadi ya Moyale Sadia Araru amewasihi wakaazi wa Kaunti ya Marsabit kuishi kwa amani wakati huu tunapokaribia uchaguzi.
Katika hotuba yake wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya Jamhuri katika uwanja wa michezo wa Marsabit hii leo Sadia amesema kuwa ni vijana ndio hutumika vibaya na wanasisa kuzua vurugu.

Amesema utata ulioshuhudiwa hivi majuzi mjini Moyale ulitokana na uchochezi wa mizingi ya kabila.
Ameomba wananchi kutoka eneo hilo kuandaa mazungumzo ili kumaliza mzozo huo.
Sadia Arura amewataka akina mama kujitokeza na kupigania nafasi zao katika nyadhifa za uongozi zilizopo.
Naye mwalikishi wadi Lokho Abduba amewarai vijana kutia bidii masomoni na kuacha matumizi ya dawa za kulevya kwani wao ndio tegemeo la siku za usoni.
Amesema kuwa uhuru unaazia akilini mwa mtu.
Amwataka wanaMarsabit pasi na migongano baina ya jamii na kufurahia uwepo wa amani hapa jimboni.
Mwakilishi wa wadi ya Sangante Adan Chukulisa ameitaka serikali ya kaunti ya Marsabit kuondoa ada ambayo hutozwa wagonjwa wanapotumia huduma za magari ya Ambulensi.
Chukuliza amesema serikali inastahili kuondoa ada hizo akisema wengi wa watu wa jimbo hili hawajiwezi kimapato na wanahitaji huduma ya magari hayo ya ambulensi.
Amesema vijana wengi hawana ajira na kuwa serikali ya jimbo inastahili kubuni nafasi zaidi za ajira kwa vijana.
Wameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya Jamhuri mchana wa leo katika uwanja wa michezo wa Marsabit.