Gavana wa kaunti hii ya Marsabit Balozi Ukur Yatani ameonya vituo vya redio vya hapa Marsabit vinavyotumiwa kueneza ukabila na kuwachochea wananchi wa Marsabit.
Gavana Yatani amesema serikali yake itatumia uwezo wa kisheria iliyonayo kusimamisha upeperushaji wa habari wa vituo hivyo.

Gavana Yatani amesema uwepo wa katiba mpya ni ufanisi kwa maeneo yaliyotengwa nyuma hususan kaskazi mashariki mwa Kenya Marsabit ikiwemo.
Gavana Yatani amesema iwapo uongozi uliopo kwa sasa ungelikuepo miaka kadhaa iliyopita jimbo hili lingelikuwa limepiga hatua kubwa kimaendeleo.
Kiongozi wa jimbo amesema kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wake serikali yake imepiga hatua kubwa ya kutiliwa mfano.
Amewapongeza wahudumu wa afya wa kaunti hii ambao wanaendeleo kuwahudumia watu wa jimbo hili.
Gavana amewakashifu wale wanaolalamikia ujenzi wa uwa unaozunguka uwanja wa michezo wa Marsabit akiwata kama watu wasiokuwa na uwezo wa kuona maendeleo yaliyoafikiwa.
Gavana Yatani amewaomba wanaMarsabit kumchagua tena kama Gavana wa kaunti hii.
Amesema muungano uliopo kwa sasa ni dhabiti na unajumuisha jamii zote za jimbo hili.