Photo; Magu Muthindika,Marsabit County Commissioner.
Akizungumza wakati wa sherehe hiyo kamishna wa kaunti ya Masabit Magu Mutindika ameonya vikali wanasiasa dhidi ya kuendeleza siasa za chuki na ukabila kuwatengaisha wananchi.
Amesema siasa duni za chuki na ukabila zimechangia pakubwa migogoro baina za jamii na kwamba serikali haitakubali kamwe uchochezi wa wanasiasa.

Amewataka wanasiasa kupiga siasa inavyopaswa na kuhubiri amani na utangamano baina za jamii.
Amesema serikali inafuatilia kwa karibu mienendo ya wanasiasa na wote wanaoeneza chuki na ukabila, na kwamba watakabiliwa ipasavyo kulingana na sheria.
Kuhusu rabsha ziliyozuka majuzi mjini Moyale, Biashara Street Mutindika amelaumu wanasiasa kwa kuchochechea jamii mbili za Burji na Garee waliokuwa wakiishi pamoja kwa muda mrefu bila uhasama wowote.
Mutindika amesema mapigano kama hayo huleta chuki na uwoga na kwamba serikali inafuatilia swala hilo kwa karibu.
Amewasihi wananchi kuheshimiana na kutokubali tena kuchochewa na viongozi wenye nia potovu.
Aidha ameuomba ujumbe wa serikali ya kaunti kushirikiana na serikali kuu katika juhudi ya kutafuta maridhiano.
Kadhalika, Mutindika ametoa onyo kali kwa vituo vya Redio katika kaunti hii ambavyo amevilaumu kwa kupeperusha matangazo za chuki na uhasama.
Ameonya kwamba iwapo vituo hivyo havitakomesha hilo na kufanya kazi kulingana na kanuni na sheria za uanahabari huenda zikapokonywa leseni zao za urushaji wa matangazo.
Kadhalika, Mutindika amechukua fursa hiyo kujibu madai kwamba jamii ya Warendille wanaoishi eneo bunge la Saku wananyanyaswa wakati wa shughuli za kusajili makurutu wa kujiunga na vikosi vya usalama nchini.
Amesema swala hilo limechangiwa na sintofahamu zilizotokea afisi kuu kule Nairobi na wanalisuluhisha kuwapa wananchi wote haki sawa.
Kuhusu barabara mpya ya Moyale-Isiolo kupitia hapa mjini Marsabit Mutindika amewataka wananchi hususan madereva wa magari na waendeshaji bodaboda kuwa waangalifu wanapotumia barabara ili kuepusha maafa ya ajali za barabarani.
Aidha, ameonya dhidi ya ujenzi ovyo wa majengo yasiyozigatia kanuni za ujenzi.
Amewaonya wanakandarasi wasiofuta kanuni za ujenzi kwamba watakabiliwa ipasavyo kwa mujibu wa sheria.
Kamishna Mutindika ametaka kamati ya kushugulikia madhara au fidia inayotokana na mashambulio ya wanyapori kuwajibika zaidi.