dsc_0195
Katibu wa kudumu katika wizara ya barabara nchini John Mosonic amezinduwa rasmi kukamilika kwa barabara ya Meriile – Moyale hapa Marsabit.
Mradi huu wa barabara ambao imefadhiliwa na Benki ya Africa ya Maendeleo ADB ulianza mwaka wa 2011 ambao imeunganisha miji ya Mombasa-Nairobi-Marsabit.
Hii ni awamu ya nne ya ujenzi wa barabara kuu ya kuunganisha Kenya na nchi jirani ya Ethiopia baada ya kitengo cha Isiolo-Merille kukamilika hapo mwaka wa 2009.
Katibu Mosonic aliwasili akiandamana na wafadhili kutoka European Union amabo ni wafadhili katika mradi huu.
Mradi huu wa jumla shilingi bilioni 9.8 na umekamilika hii leo ambapo lami ya mita mia moja imeshuhudiwa ikamilika na kuzinduliwa na katibu Mosonic na Gavana wa kaunti ya Marsabit Ukur Yattani.
Gavana Ukur amesema wanaMarsabit wamesubiri kukamilika kwa barabara hii akiongeza kuwa sasa barabara hiyo italeta maendeleo ya kibiashara hivyo kuinua uchukuzi wa kaunti hii.
Aidha Gavana Ukur ameongeze kusema kuwa serikali yake na ya kitaifa zimeanda mazungumzo na rais Uhuru Kenyatta ili kufanikisha ujenzi wa barabara ya lami kuelekea Segel kuliko mradi wa kichingio ili  kurahisisha uchukuzi wa mifugo na nyama na bidha za wanyama.
Kupitia Mazungumzo ya Gavana Ukur na Rais Kenyatta barabara mpya ya lami itajengwa kutoka eneo la Laisamis na kuelekea Serima kwenye mradi wa Lake Turkana Wind Power.
Aidha barabara za hapa mjini Marsabit zitawekwa lami hivi karibuni.
Gavana Ukur amesema kuwa serikali imetenga fedha za kuboresha mji wa Marsabit na mitaa yake kuwa ya kisasa kupitia mradi wa kuweka taa za barabarani yaani streetlights na bomba ya kupitisha maji taka.