PICHA: Maadimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika eneo la Moyale, Kaunti ya Marsabit.
Mwandishi: Adano Sharawe.
TAREHE 21/09/2018: Wito wa amani umeshamiri katika maadhimisho ya kimataifa ya siku ya amani ulimwenguni yaliyoandaliwa mjini Moyale.
Naibu gavana Solomon Riwe ambaye alikuwa mgeni mheshimiwa ametoa wito kwa wenyeji jimboni kujiepusha na chuki, ukabila na tetesi duni zisizo na maana ambayo anasema huchangia mizozo baina za jamii. Baadala yake Riwe amewataka wenyeji kuangazia ajenda muhimu zitakazowafaidi kama wenyeji wa jimbo hili kuleta maendeleo.
Akihutubia wenyeji katika ukumbi wa Baraza Park, mjini Moyale Riwe ametoa changamoto kwa makundi yote ya jamii kujitolea kikamilifu kuunga mkono juhudi za serikali za kitaifa, kaunti na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kueneza amani. Kulingana na naibu gavana wananchi wanajukumu kubwa la kuhakikisha wito wa amani unatekelezwa kwa vitendo.
Riwe alichukua fursa hiyo kupongeza hatua kubwa anayodai zinatelelezwa na wazee wa amani mjini Moyale kwa kujitolea kuwa nguzo kuu ya kuleta maridhiano na mapatano baina za jamii mjini humo.
Amewataka wazazi pia kuwa kielelezo chema kwa watoto wao kwa kuwaandalia mazingira bora ya malezi yatakayowasaidia kuelewa athari za mizozo na faida za amani wangali wadogo.
Vile vile, naibu gavana ametambua mchango wa imani ya dini mbali mbali kuleta maafikiano, akiwapa changamoto wananchi kuishi kulingana na mafundisho ya dini zote ambayo anasema ni amani na upendo.
Kauli yake ilikaririwa na naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Moyale.
Hafla ya mwaka huu inajiri wiki chache tu baada ya watu wawili kuuwawa huku wanne wakijeruhiwa kufuatia mapigano ya kikabila kwenye kitongoji cha Horender, eneo bunge la Saku.
Kwa upande wake afisa wa shirika lisilokuwa la kiserikali la PACIDA, ambayo ni kati ya mashirika yaliyofadhili hafla ya leo ametoa himizo kwa wenyeji wa Moyale na kaunti kwa ujumla kuzika tofauti za kikabila na kuendelea kukumbatia amani kwa ajili ya umoja na ushikamano za kijamii na zaidi kuafikia maendeleo.
Hafla ya leo imeandaliwa kupitia ushirikiano za shirika la PACIDA pamoja na mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya kiserikali hapa jimboni, serikali ya kitaifa na ya kaunti ya Marsabit.
Kauli mbiu ya siku ni ‘Haki kwa amani
Katika maadhimisho ya amani duniani, naibu gavana wa kaunti ya Marsabit bwana Solomon Riwe amewahimiza wananchi kushiriki kikamilifu midahalo kuhusu miradi ya seikali kila mara inapoendeshwa na serikali ya kaunti.
Riwe amesema hiyo ndiyo njia pekee ya wananchi kuhakikisha sauti zao zinasikikika kuhusu miradi inayofaa kupewa kipaumbele na kutekelezwa na serikali.
Amelalamikia kasumba anayosema inashuhudiwa kila mara jimboni wakati wa midahalo hiyo kuhusu miradi ya serikali inapoaandaliwa ambapo watu wachache hujitokeza kushiriki.