NACC marsabit
Serikali ya kaunti ya Marsabit ikishiriakana na kamati ya National Aids Control Council hii leo imezindua mradi wa kupambana na jinamizi la ugonjwa wa ukimwi.
Hafla hii ya uzinduzi ilifanyika katika mkahawa wa Imperial Dale hapa Marsabit imewaleta pamoja wafanyakazi kutoka wizara ya afya,watu waonaishi na virusi vya ukimwi na viongozi kutoka serikali ya kaunti.
Kuligana na ripoti ya mwaka wa 2015 maabukizi mapya imeongezeka hadi kufika asili mia moja nukta nne katika kaunti ya Marsabit.
Watu takriban 2841 wanaishi na virusi vya ukimwi katika kaunti hii ya Marsabit kuligana na ripoti ya NACC.
Kila mwaka watu 11 katika kaunti ya Marsabit wanaambukizwa virusi hizi ya ugonjwa wa ukimwi katika kaunti hii ya Marsabit.
Mpango wa kupigana na ugonjwa wa ukimwi inanuia kutoa mwelekeo wa miaka mitatu 2016-2019 ambao kaunti ya Marsabit ni ya 24 kutoa katika nchi ya Kenya.
Insert Labarakwe.
Naibu Omar Ali alisema ni jukumu letu zote kupigana na jinamizi hilo hata kule mashinani na serikali imejitolea kwa kusaidia na mashirika kama NACC.