​Jamaa mmoja anazuiliwa kwa sasa na maafisa wa kukabiliana na ufisadi EACC kule Isiolo baada yake kupatikana akitoa mlungula kwa afisa wa IEBC
Jamaa huyo kutoka hapa Marsabit,anadaiwa kuwa alikua ameenda kukutana na afisa huyo wa IEBC katika mkahawa mmoja kabla ya kufumaniwa na maafisa hao
Kulingana na Ignatius wekesa ambaye ni mkuu wa tume ya EACC ukanda wa mashariki mwa Kenya,jamaa huyo alikua anataka afisa wa IEBC kuwaajiri watu Fulani wapatao 46 katika eneo bunge la hapa Marsabit ambao watasimamia uchaguzi ujao.
Wekesa Aidha,amesema kuwa,shilingi elfu 200 zimepatikana kutoka kwa mshukiwa pesa ambazo anadaiwa kuwa,alikua anataka kupeana kama hongo kwa afisa huyo.
Eacc pia ainasema kuwa,inaendeleza uchunguzi zaidi kuhusu kisa hicho na baadaye watawasilisha uchunguzi wao kwa afisi ya mkurugenzi wa mashtaka keriako tobiko ili hatua zichukuliwe kwa mshukiwa.
Duru za kuaminika zinasema kuwa,mshukiwa ana uhusiano wa karibu na mwanasiasa Fulani jimbo hili la Marsabit.