Picha: Binduki aina ya HK 21,Risasi 184.

Mshukiwa mmoja wa uhalifu amekamatwa eneo la Shur kaunti ndogo ya Maikona jimbo hili la Marsabit akiwa na silaha bila kuwa na leseni ya umiliki.

Alikamatwa na bunduki aina ya HK 21 na risasi 184 akiwa nyumbani kwake mwendo wa saa tatu asubuhi.
Mshukiwa huyo anahusishwa na visa vya mauwaji vilivyotokea eneo hilo wiki kadhaa zilizopita.
Kwa sasa mshukiwa anazuilinwa na na polisi katika kituo cha polisi cha Marsabit huku akiwasaidia polisi kufanya uchunguzi zaidi.

Polisi walipata taarifa kutoka kwa wenyeji wa sehemu hiyo na kisha kumfumania na kumkamata.