PICHA: Wahamiaji kutoka nchi jirani ya Ethiopia wakitafuta msaada Moyale,Kenya
 
Hofu ya mkurupuko wa ugonjwa wa kipindupindu inakisiwa kuanza kwenye makambi ya wakimbikizi eneo la moyale jimbo hili la Marsabit.
Haya ni kwa mujibu wa naibu gavana wa jimbo hili Solomon Riwe.

 
Kwenye kikao na kituo hiki mjini Moyale,Riwe amesema kuwa,hali hiyo ni kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoingia nchini, baada ya hali tete ya kiusalama kushuhudiwa nchini Ethiopia.

 
Aidha,naibu gavana amesema kuwa,hali duni ya mazingira wanakokita kambi kwa sasa wakimbizi hao  ni mbovu,akisema kuwa,hawana vyoo vya kutumia kwa sasa.
 
Wakati uohuo,Riwe amesema kuwa,serikali ya kaunti inaendelea kutoa msaada kwa waathiriwa hao, japo anahoji kuwa,msaada huo hautoshi kamwe.

 
Tangu vikosi vya usalama nchini Ethiopia kuwapiga risasi na kuwauwa watu 15 papo hapo,hali ya usalama imeendelea kuwa ya wasiwasi nchini humo, huku wengi wa wakaazi wakitorokea mjini moyale kwa usalama.
 
Kulingana na naibu gavana Riwe,ni kuwa idadi kubwa ya wakimbizi hao ni watoto na kina mama huku idadi hiyo ikikisiwa kuwa 8200 kufikia leo.

 
Kuhusu iwapo watajenga kambi moja ya kuwasitiri wakimbizi wote,naibu gavana amesema kuwa,majadiliano yanaendelea ili kubaini sehemu watakapojenga kambi hiyo.
Kwa sasa wakimbizi hao wako kwenye maneneo ya Sesi,Butiye,dambalafachana na Somare.
 
 
 
 
 
Facebook: Radio Jangwani News Today
Twitter: Jangwani 106
Website: www.radiojangwani.co.ke
©RADIO JANGWANI 2018