dsc_0065
Mgomo wa madaktari unaoshuhudiwa kote nchini umeathiri pakubwa shughuli za huduma za Afya na matibabu katika hospitali ya rufaa ya Marsabit.
Madaktari katika hospitali hiyo ya kipekee hapa jimboni wamegoma hivyo kutatiza huduma hospitalini hapa.

Wagongwa waliolazwa katika hospitali hiyo wanahangaika wasijue la kufanya huku wenye uwezo wa kimapato wakiwapeleka jamaa zao katika hospitali za kibinafsi kupata matibabu.
dsc_0061
Wagonjwa waliathirika zaidi ni wale waliolazwa katika vyumba vya kujifungulia akina mama,wanaohitaji upasuaji,watoto wachanga na wale wanaohitaji uangalizi wa madaktari baada ya kupokea matibabu.
Shajara ya radio jangwani imepata nafasi kuzungumza na mgonjwa mmoja ambaye alilazwa katika hospitali ya rufaa ya Marsabit na kunielezekea mateso wanaopitia.
dsc_0062
Baadhi ya madaktari wa hospitali kuu ya Rufaa ya Marsabit wamesafiri kuelekea jijini Nairobi kujiunga na wenzao katika ngomo huo.