Photo: Laini ya stima KETRACO katika kaunti ya Marsabit.
Mfanyikazi mmoja wa kampuni ya kutengeneza barabara ya KETRACO amefariki baada ya kuangukiwa na chuma.
Taarifa zinasema mfanyikazi huyo mwenye asili ya hindi ameaga dunia baada ya chuma iliyokuwa imebebwa na Kreni kuteleza na kumwangukia,Chuma hicho kimesasbabisha shimo kubwa tumbo na kumpeleka kufanja damu nyingi.
Amefariki alipokuwa akikimbizwa kupokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Marsabit.
Kisa hicho kimetokea jioni ya leo karibu na kijiji cha Jirime ikioko kilomita chache nje ya mji wa Marsabit.
Kimetokea wakati wafanyikazi wa kampuni ya KETRACO walipokuwa wakijenga nguzo ya nyaa ya stima.
Mwili wake umelazwa katika chumba cha kuifadhi maiti katika hospitali ya Rufaa ya Marsabit.
Kampuni ya KETRACO inatengeneza laini ya stima kando ya barabara kuu ya inayounganisha mji wa Marsabit na Isiolo.
Wanahabari wetu kwa sasa wako katika hospitali ya rufaa ya Marsabit ili kukuletea taarifa hio kwa utendeti.