Picha:John Tate,Mliki wa Kliniki ya Marsabit Medical Clinic,Kaunti Ya Marsabit.
Wamiliki wa kliniki hapa mjini Marsabit wanalalamikia kumwagwa kwa uchafu wa hospitali maeneo ya kliniki zao.
Wamiliki hao wandai hiyo ni njama ya baadhi ya wenye hospitali kubwa hapa mjini Marsabit wakiwa na nia ya kutaka kliniki zao zifungwe na wahudumu wa afya.
Wakizungumza na Radio Jangwani wamesema sio mara ya kwanza njama kama hiyo kutokea na kupelekea kufungwa kwa baadhi ya kliniki za kibinafsi.
John Yate mmilikiwa wa kliniki ya Old Is Gold iliyoko hapa mjini anasema alipigwa na butwaa alipofika kazini asubuhi ya leo na kupata taka karibu na kliniki yake.
Wametoa lalama zao kwa idara ya polisi na kuitaka idara hiyo kufanya uchunguzi wa kina ili kuwanasa wenye nyama hiyo ya kusambaratishi kazi zao.
Wagonjwa wanaotafuta huduma katika kliniki hiy wamesema kitendo hicho cha kutupa taza za hospitali kiholela ni hatari kwa afya ya wanamarsabit.
Wafanyikazi wanaohudumu eneo hili walikashifu kitendo hicho.
Aidha wamiliki hawa wameomba idara ya polisi kuharakisha uchunguzi huo.