Mradi wa kuteka maji kutumia technolojia ya kisasa ya ATM umeleta manufaa mengi kwa wakaazi wa mji huu wa Marsabit.
Shirika la FH Kenya kwa ushirikiano na PACIDA ndio wahisani ambao wanefadhli mradi huo wa kuteka maji kwa njia hiyo ya kielektroniki.
Kwa miaka mengi sasa sekta ya maji katika mtaa huu wa marsabit umekumbwa na changamoto chungu nzima na sasa mradi huo umeleta mabadiliko mengi.
Mradi huo wa maji unasimamiwa na kikundi cha Sakuu Welfare for Disables ambacho kinajumuisha watu ambao wanaishi na ulemavu.
Kituo hicho cha kisasa cha kuuza maji kinapatikana karibu eneo la Huduma Center hapa mjini Marsabit.
Akizungumzana radio jangwani  Zangabo Hussein amesema kuwa wanapata maji safi kwa bei ya chini na technolojia hio mpya imerahisha shughuli nzima ya kuchota maji.
 Ili kuteka maji mnunuzi anafaa kuwa na kidubwasha fulani cha kielektroniki ambacho huwekwa mjazo wa pesa.
Kidubwasha hicho kisha huelekezwa kwenye mashine ya kielektroniki sehemu ya kutekea maji ambayo ina uwezo wa kuwasiliana na kidubwasha chenyewe na kisha maji yanaweza kutiririka baada ya mfereji kufunguliwa.
Mnunuzi anaweza tu kuteka maji  mitungi 5 ya lita 20 kwa siku kwa gharama ya shilingi 50.
Hatua hiyo imechukuliwa ili kuhakikisha kuwa kila mnunuzi anaweza kuteka maji.
Mradi huo imegharimu shilingi million saba.