PICHA: Wanafunzi wa vyuo vikuu katika ukumbi wa Kanisa Katoliki, Marsabit
Wanafunzi wa vyuo vikuu katika kaunti ya Marsabit kwa sasa wanaandaa warsha ya mazungumzo kuhusu masaibu wanaokumbana nayo wanapoendelea na masomo yao.
Wanakutana chini ya miavuli mbali mbali ikiwemo Baliti University Students Association – BUSA, Rendile University Students Association RUSA, Samburu University Students Association – SUSA na Muslim University Students Association –MUSA.
Katika kungamano hilo linaloandaliwa katika ukumbi wa kanisa Katoliki hapa Marsabit wanafunzi hao wametaja ukosefu wa nafasi ya kujifunza kazi yaani Internship, ukosefu wa karo kwa wanafunzi maskini na matumizi ya dawa za kulevya kama mojawapo ya masaibu na changamoto zinazowakumba.
Akizungumza na Radio Jangwani mwenyekiti wao Hussein Tiri wamekutana kama wanavyuo kutoka maeneo mbali mbali ya kaunti hii ili kuzumgumza kwa pamoja na kutafuta  suluhu ya changamoto wanazo kumbana nazo.
 
Naye Mwenyekiti Wako Sora amesema kuwa muungano huo wa wanafunzi ni bora zaidi kwa wamepata fursha ya kutangamana na kuzungumza kwa pamoja kama wanafunzi.
Wameomba serikali ya kaunti,kitaifa na mashirika yasiokuwa ya kiserikali kuwapa wanafunza fursa ya kujiendeleza kwa kujifunza talumazao katika idara zao mbali mbali.