Kizaazaa kimeshudiwa katika kituo cha polisi hapa Marsabit baada ya mgombea kiti cha mwakilishi wadi eneo la Marsabit Central Hassan Wako almarufu Mila dhema kuzuiwa kwa muda na polisi wa kituo cha Marsabit.
Mila Dhema aliamurikwa kufika kituo hicho baada ya aliyekuwa kansela wa  eneo la Marsabit Central Kalish Hukka kuandikisha taarifa kuwa Mila-Dhema amemtishia maisha.
Wananchi waliojawa na ghadabu walifurika kituo hicho huku wengine wakilia na kupiga mayowe wakitaka kumwona kiongozi wao.

Akizungumza na Radio Jangwani katika kituo cha Polisi Mwakilishi wadi mteule kutoka eneo la Moyale Sadia Araru amesema viongozi hao wawili wanastahili kuondoa kesi hiyo na kwenda kutafuta suluhu nje kama jamii mmoja.
Kwa sasa idara ya polisi inaendelea kuchunguza kesi hiyo huku viongozi hao wawili wakijadiliana kwa usaidizi wa wazee ili kupata suluhu.
Taarifa zinasema utata baina ya wawili hawa ni wa kisiasa.