PICHA: Gavana Ali akipokelewa na densi ya kitamaduni wadi ya Sagante, Kaunti ya Marsabit.
TAREHE 05/08/2018-Gavana wa jimbo hili Muhamud Ali ameanza rasmi ziara yake ya kutembelea wadi kadhaa jimboni kwa ajili ya kutathmini miradi iliyofanikishwa tangu achukue usukani wa uongozi, kando na kutoa shukrani zake kufuatia kuchaguliwa kama gavana katika uchaguzi uliopita.
Wenyeji wa eneo bunge la Saku kwenye wodi ya Karare na Sagante/Jaldesa katika jimbo hili la Marsabit kuanzia siku ya Ijumaa walimpokea Gavana Ali na ujumbe wake wa maafisa wa serikali ya kaunti, pamoja na viongozi wengine wa
Kaunti hii ya Marsabit.
Wakizungumza wakati wa hafla hiyo, wenyeji wa wodi Karare na Sagante walichukua fursa hiyo kuelezea miradi wanayopania kutekelezwa katika wadi hiyo.
Mwakilishi wadi wa Karare Stephen Leado amesema mengi yamefanikishwa chini ya muda mchache serikali ya gavana Ali imehudumu.
Leado amemwomba Gavana Ali kuhakikisha idara zote za serikali ya kaunti inafanya uhamasisho ya kutosha kwa wananchi hususan kuhusiana na ukuuaji ma mji kama ilivyopendekezwa na bunge la kaunti ya Marsabit.
Kwa upande wake Mwakilishi wodi wa Sagante/Jaldesa Sora Katelo amempongeza serikali ya kaunti chini ya uongozi wa Mohamud Ali kwa utendakazi wake kwa wakaazi sehemu yake katika idara mbalimbali huku akiwahimiza wanaSagante kuwa kipau mbele katika kilimo biashara kama njia moja kujiinua kimaisha.
Wakati huo huo mbunge wa Saku Dido Rasso ameelezea matumaini yake kwamba serikali ya kaunti kwa ushirikiano na viongozi wa eneo hilo itajaribu kupata mwafaka kwa matatizo mbalimbali inayokumba hususan wenyeji wa wodi ya Karare na Sagante Jaldesa.

Rasso ameomba Gavana wa jimbo hili kuhakikisha bidii katika utendakazi wa miradi mbalimbali za idara zote jimboni.
Raso ametoa mfano wa swala la maji na ardhi ambayo amesema ni muhimu kwa mwafaka kuafikiwa baina ya wenyeji na idara ya huduma kwa wanyamapori nchini KWS ambapo ameeleza kwamba kuna mpango wa kuhakikisha sehemu ya ardhi hiyo inarudishwa chini ya umiliki wa jamii ya Karare, Amesema watapeleka mswada katika bunge la kitaifa na seneti kufanikisha hilo.
Naye seneta Abubakar Harugura ameeleza kwamba ni jambo la busara kwa ziara kama hiyo kufanyika kutoa fursa kwa wenyeji kutangamana na viongozi wao na kusikia moja kwa moja kutoka wananchi.
Harugura pia amewasihi wakaazi wa Badassa na Dirib kwenye wadi ya Sagante kuimarisha ukulima bora kando na mabadiliko ya hali ya anga hasa wakati was msimu unaokuja.
Hargura amehoji kwamba mwaka moja baada ya uchaguzi viongozi wa jimbo hili wamesimama kidete kwa maswala ya kimaendeleo na ushirikiano wa kulinda maslahi ya kila jamii akitoa mfano wa kesi iliyowasilishwa mahakamani kupinga unyakuzi wa ardhi ya jamii ya Warendile anaodai ilinyakuliwa kwa njia isiyofaa, kwa ajili ya ujenzi wa mradi ya kawi kutokana na upepo eneo la Loiyangalani.
Gavana Mohamud Ali kwa upande wake alichukua fursa hiyo kugusia baadhi ya miradi za kimaenedeleo inayofanikishwa kwa sasa na serikali yake katika mud
Ameeleza kwamba serikali ya kaunti itawahudumia wananchi wote jimboni kwa usawa bila ubaguzi wa aina yeyote.
Gavana Ali ametoa shukrani kwa wenyeji kwa kumpa nafasi ya kuwaongoza.
Amewaomba wenyeji wa Karare na Sagante Jaldesa kwenye eneo bunge la Saku jimbo hili kwa ujumla kutopotoshwa na propaganda duni inayoendeshwa na baadhi ya wanasiasa kwa ajili ya kuhujumu utendakazi wa Serikali yake, Gavana Ali amesema serikali yake imejitolea zaidi kulinda haki kwa wote, kuimarisha usalama na amani jimboni kufanikisha maendeleo.
Kuhusu afya Gavana Ali amesema mradi wa bima ya afya ya NHIF ni mojawapo ya miradi kuu inayoangaziwa na serikali yake kwa ajili ya kuwaondolea wenyeji hususan wasiobahatika katika jamii gharama ya juu ya matibabu, Kando na hayo ameongezea kwamba magari 10 za ambulensi ziko tayari kuhudumia wananchi bila ya mwananchi kutozwa ada yoyote.
Amesema magari mawili ya ambulensi pamoja na vifaa vya hospaitali ambayo alipewa na wafadhili kule merikani yatafika kwa kipindi cha mwezi moja ujao.
Kuhusu elimu Gavana Ali amesisitiza kwamba serikali ya Kaunti imeweka mikakati kabambe kuona kwamba wanafunzi wote hususan wasiojiweza kifedha wanapata nafasi ya kuendeleza masomo yao kwa kupata ruzuku ya mosomo kutoka serikali ya kaunti.
Kulinga na na Gavana Ali mradi huo unawalenga wanafunzi punde baada ya kukamilisha shule ya msingi ama upili.
Kuweza kufaulu kupata ruzuku hiyo serikali ya kaunti imeweka masharti kwamba kila mwanafunzi atakayejizolea alama 350 na zaidi kwa wavulana na 300 na zaidi kwa wasichana katika mtihani wa kitaifa wa shule ya msingi KCPE atalipiwa karo na serikali ya kaunti.
Kwa wanafunzi wa shule ya upili, mtahiniwa sharti ametimiza alama ya B- ama zaidi kwa wavulana na C+ ama zaidi kwa wasichana kupata nafasi hiyo ya kulipiwa karo na serikali ya kaunti, Aidha, ameongezea kwamba serikali yake itasimamia kikamilifu karo ya wanafunzi watakaojiunga na taasisi za kiufundi.
Wakati huo huo katika ziara yake ya kutembelea wodi hizo mbili kwenye eneo bunge la Saku Gavana amewahidi wakaazi wa Karare kwamba serikali yake imejitolea kwa ujenzi wa bweni la shule ya upili was mseto wa Karare.huku akitoa ahadi ya kujenga afisi ya mwalimu mkuu kwa shule ya msingi wa badassa, shule ya Upili wa Badassa na St.Peter’s kwenye wodi ya Sagante Jaldesa.