Watu watatu akiwemo afisa mmoja wa polisi wa utawala AP wamethibitishwa kufariki baada yao kumiminiwa risasi na watu wasiojulikana katika benki ya equity tawi la Elwak katika kaunti ya mandera mapema hii leo.
Kulingana na kamishna wa kaunti ya mandera Fredrick shisia,tukio hilo linadaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa alshabaab ambao baadaye walitorokea taifa jirani la Somalia.
Shisia amesema kuwa,kwa sasa wameimarisha doria mjini mandera na viunga vyake huku wakiwatafuta waliotekeleza uvamizi huo.
Aidha,amesema kuwa,waliotekeleza mauaji hayo walitorokea bura hache kwa kutumia gari dogo aina ya probox ambalo anasema kuwa,halikua na nambari ya usajili