PICHA: Mbunge wa North Horr,Chachu Ganya,Wakati wa uzinduzi wa chama cha FAP,Kaunti ya Marsabit.

Mbunge wa North Horr Francis Chachu Ganya ametangaza kuwa atastaafu siasa mwaka 2022.

Kwenye mkao na wanahabari eneo la Bubisa hivi leo Ganya amesema iwapo atateuliwa tena kama mbunge wa North Horr,atakamilisha muhula wake na kasha astaafu.

Mbunge huyo amesema ametekeleza mengi ya kuigwa na kuwa ana imani ya kuchaguliwa tena kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Aidha Ganya amesema atashirikiana na serikali ya kaunti katika zoezi la kuwanunua na kuwachinja mifugo waliodhoufika ili kuwafaidi wafugaji ambao wamekua wakiwapoteza mifugo wakati wa ukame.

Kuhusu elimu Ganya amesema kuwa, tayari ameanzisha wakfu wa Chalbi ambao unawalipia wanafunzi karo ya shule.

Ganya ameyasema haya katika mkutano wa kisiasa unaoongozwa na gavana Ukur Yatani eneo la Bubisa,Kaunti ya Marsabit.