PICHA: Wakimbizi katika kambi ya Somare eneo bunge la Moyale.
Serikali imefunga rasmi kambi ya wakimbizi ya Somare eneo bunge laMoyale jimbo hili la Marsabit.

Akiongoza hafla hiyo kambini humo, gavana wa jimbo hili Muhamud Ali amesema kuwa hatua ya kufunga kambi hiyo imetokana na agizo la serikali ya kitaifa.

Gavana Muhamudamewataka wakimbizi waliosajiliwa na shirika la kuwashugulikia wakimbizi la UNHCR kukubali wito wa kupelekwa katika kambi kubwa ya wakimbizi ya Kakuma ilioko katika kaunti yaTurkana.

Aidha amewarai wakimbizi ambao walikwepa kusajiliwa kurejea makwao.

Mkuu huyo wa kaunti amefafanua kuwa sasa wakimbizi hao watakua chini ya uangalizi wa serikali ya kitaifa, na baraza la kuwashugulikia wakimbizi duniani RASyaani Refugees Affairs Secretariat.

Wakati huo huo Gavana Muhamud Aliameyashukuru mashirika ambayo yamekua yakitoa msaada kwa wakimbizi hao katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Gavana Muhamud alikuwa ameandamana na wabunge Ali Rasowa eneo bunge la Sakuna Mbunge wa Moyale Qalicha Gufu.

Baadaye gavana alielekea kambi yaDambalafachana mojawapo ya kambi inayotumika kwa sasa kuwasitiri wakimbizi kabla yao kusafirishwa hadi Kakuma hivi karibuni.

Inakisiwa kuwa karibia wakimbizi alfu 15 walivuka mpaka wakitokea Ethiopia na kuingia nchini eneo la Moyale baada ya wao kuhofia maisha yao kufuatia mauwaji ya raia na vikosi vya usalama nchini humo.