Muungano wa madhehebu ya kipentekosti hapa jimboni Marsabit MPF, sasa unashinikiza serikali kuwakabili matapeli wanaodaiwa kuvamia na kunyakuwa ardhi ya makaburi ya wakristo hapa jimboni kwa miradi yao ya kibinafsi.

Wakizungumza na kituo hiki wakati wa kuanza maandamano ya Amani hadi kwenye afisi ya kamishna wa kaunti hii,mwenyekiti wa muungano huo William Godana amesema kuwa,hatua hiyo inafuatia notisi kwenye gazeti rasmi la serikali kutaka mabwenyenye hao kutoka kwenye ardhi hiyo.

Naye naibu mwenyekiti wa MPF Rev. Diba Said anasema kwamba wanaitaka serikali kuingila kati na kulazimisha ardhi hio kurejeshwa kwao,kwani wamefuata mkondo wa sheria lakini hakuna linalofanyika.

Maandamano hayo yanatarijwa kukamilika baada yao kukutana na kamishna wa kaunti hii, ili kutanzua hali hiyo ambayo huenda ikalemaza shughuli katika eneo hilo ya makaburini.