Wananchi jimboni wamehimizwa kujitolea zaidi kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Wito huo umetolewa wakati wa siku ya mazingira duniani ilioadhimishwa katika kituo cha kibiashara cha Hurri Hills eneo-bunge la North Horr.
Washikadau walioudhuria hafla hiyo walielezea kusikitishwa kwao na kupungua kwa kiwango cha misitu jimboni.
Shughuli za kibinadamu na ukosefu wa mafunzo kuhusu uhifadhi wa mazingira umelaumiwa pakubwa kama miongoni mwa sababu kuu zinazochangia hali hii.
Aina ya mti unaojulikana kisanyansi kama Osyris Leciolata na Wato Qayya kwa lugha ya kiborana umetajwa kama ulio kwenye athari ya kuangamia jimboni.
 Shughuli hiyo ya maadhimisho iliendeshwa na shirika la Pacida kwa ushirikiano na shirika la kimataifa la Maltezer International.
Washiriki wengine ni mamlaka ya mazingira nchini Nema na maafisa wa huduma ya misitu nchini KFS, shule za msingi ya Hurri Hills na Baqaqa pamoja na wananchi wa tabaka mbalimbali kutoka eneo hilo.
 
Shirika la Pacida limesema linashirikisha jamii katika uhifadhi wa mazingira kwa kuwapa miche ya kupanda ambapo kufikia sasa zaidi ya miche 2000 imepandwa eneo hilo.
 Akizungumza kwenye hafla hiyo, mkurugenzi mkuu wa shirika la Pacida Katello Isacko amewaomba wananchi kujiepusha na ukataji ovyo wa miti na kukumbatia juhudi la shirika hilo la kutunza mazingira.
Amewafahamisha kwamba kupanda miti zaidi na kutunza mazingira ndizo njia pekee ya kukabiliana na athari ya mabadiliko ya hewa.
Kauli yake ilikaririwa na mkurugenzi wa shirika la Nema jimboni Simón Tonui aliyewarai wananchi kujiepusha na uchafuzi wa mazingira.
Amesema sheria ni wazi kwamba atakayepatikana akichafua mazingira atakabiliwa na kuadhibiwa kwa mujibu vikali.
Kauli mbiu ya siku ni tusimame na mazingira.