Leo ni siku ya choo duniani inayoratibiwa na Umoja wa Mataifa huku kukitolewa wito wa kuboresha mazingira na kuzingatia usafi wa vyoo vyenyewe. 
Siku hii ya choo duniani inakumbusha ulimwengu kuwa watu zaidi ya bilioni 2.5 duniani kote wanakabiliwa na matatizo yanayoambatana na ukosefu wa vyoo vinavyokithi mahitaji ya wakati hatua ambayo inawaweka kwenye mazingira ya kukumbwa na matatizo ya kiafya.
Ripoti moja iliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuambatana na siku hii inawataja wanawake na wasichana kuwa ndiyo walioko kwenye kundi hatarishi la kukumbwa na matatizo ya kiafya na inataka kuwekwa msukumo wa kubadili hali hiyo.
Hayo yakijiri aliyekuwa Miss Tourism 2013 kaunti ya Marsabit Bi Qabale Duba ametoa wito kwa Serikali ya kaunti pamoja na washika dau mbalimbali kutengeza vyoo vya uma kwa wingi ili mtoto wa kike apate kujisitiri anapokuwa katika kipindi cha hedhi.
Bi Qabale ameyasema hayo katika Warsha ya kuwahamasisha akina mama kuhusu PAPA Project Eneo la Hula hula Kaunti Ndogo ya Saku.
Kwingine Shirika la Caritas Marsabit imeanda sherehe ya siku ya leo eneo la Loiyangalani katika kijiji cha Komote,kijiji hicho ni maeneo yanayoathirika pakubwa kutoka na hali duni ya usafi.