Picha:Njoroge Waweru,Meneja Msimazi wa sekta ya mifungo katika shirika la ILRI akichanja mbuzi eneo la Merille,Kaunti ya Marsabit.
Wafugaji wa jimbo hili wametakiwa kuhakikisha kuwa wanawachanja mifugo yao mara kwa mara ili kuepuka hasara kupitia magonjwa mbali mbali.
Akizungumza wakati wa sherehe ya kuzindua chanjo ya mifugo eneo la Merille, Meneja wa mifungo katika shirika lisilo la Kiserikali ya ILRI Njoroge Waweru amesema kuwa chanjo ya mara kwa mara husaidia mifugo dhidi ya magonjwa na kusaidia familia husika kimapato.

Ameshauri wenyeji kushirikiana na maafisa wa shirika la ILRI na wadau wengine kufanikisha chanjo ya mifugo katika jimbo hili ambao imegharimu shilingi milioni mbili.
Kuna haja ya wadau mbali mbali kushirikiana na serikali ya kaunti katika maswala ya chanjo ya mifugo jimboni.
Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi katika wizara ya mifugo Boku Bodha.
Akizungumza wakati wa kuzindua chanjo ya mifugo eneo la Merille hii leo,Daktari Boku ametoa wito kwa mashirika mengine kuweka mikakati ya kushirikiana na serikali ya kaunti haswa katika sekta ya uvuvi na ufugaji.
Ameomba wenyeji kuhakikisha kuwa mifugo yao wanapata chanjo ili kukinga mifugo dhidi ya madhara ya aina yoyote.
Hata hivyo Mathew Lechipan Naibu Msimazi wa Kaunti ndogo ya Laisamis  ameangazia umuhimu wa wazazi kuhakikisha kuwa watoto wa kike wanapewa kipaumbele ili kuwaokoa kutokana na madhara mbali yanayowakabili kuliko watoto wa kiume.

Ameongezea kuwa mzazi yeyote ambaye anadhulumu mtoto wa kike atachukuliwa hatua za kisheria.
Pia amedokeza mtoto mtoto wa kike kupewa kipau mbele hakumaanishi mtoto wa kiume anatekelezwa.
Uchumi wa mifugo unatarajiwa kukuwa kwa asilimia 50 kufikia mwaka wa 2018 katika jimbo hili.
Aidha zaidi ya familia 60,000 zinatarajiwa kujikomboa kutokana na lindi la umaskini kupitia biashara ya mifugo pamoja na kuinua kiwango cha lishe bora.
Haya ni kulingana na mpango wa Kenya Accelerated Value Chain Development Livestock Component mwaka wa 2017.
Mpango huu unaongozwa na shirika la ILRI kwa ushirikiano na FEED THE FUTURE kutoka kwa watu wa wamerekani na serikali ya kaunti ya Marsabit.