Shirika la Caritas Marsabit hii leo imeadimisha siku ya choo duniani katika eneo la Loiyangalani,Kijiji cha Komote.

Tarehe 19 mwezi Novemba kila mwaka ni siku ya choo duniani. Kiasi ya watu bilioni 2.5 duniani hawana vyoo salama na vya kisasa na wengine bilioni moja hawana choo kabisa.
Kijiji cha Komote ilioko eneo la Loiyangalani ni moja ya vijiji inayoatirika pakubwa na tatizo la kutokuwa na vyoo salama,kijiogorafia kijiji hicho iko kando mwa ziwa turkana hivyo basi hali ya usafi ni duni.

Komote Village, Loiangalani. One of the area most affected by poor Sanitation diseases like Cholera
Komote Village, Loiangalani. One of the area most affected by poor Sanitation diseases like Cholera

Changamoto ya tatizo la kutokuwa na vyoo katika maeneo mengi mashinani inatokana na gharama kubwa ya vifaa vya ujenzi, umasikini na ufukara wa wananchi kutokana na kipato duni na kiwango cha uelewa,na hali ya miamba na baadhi ya maeneo kuwa na chemichemi nyingi hasa mabondeni.

Kulingana na umoja wa Mataifa ,kila mwaka zaidi ya watoto 800,000 walio chini ya umri wa miaka mitano hufa kutokana na kuharisha, chanzo kikuu kikiwa ni ukosefu wa usafi.

Ukosefu wa vyoo visafi mashuleni pia unawazuia watoto wengi hasa wa kike kushindwa kusoma vizuri hasa baada ya kuvunja ungo. Shule zilizo na vyoo vizuri vinachangia asilimia 11 ya wasichana kuhudhuria masomo.

Wanawake pia walio na hakikisho la kuwa na faragha na usalama wanapokwenda haja,hawako katika hatari ya kushambuliwa na kubakwa ikilinganishwa na wasio na vyoo.

Hata hivyo himizo linatolewa kuhakikisha ujumbe wa umuhimu wa kuwa na vyoo,kujua kuvitumia vizuri na kuwa na vyoo katika maeneo salama unawafikia watu bilioni 2.5 kote duniani ambao bado wanakosa huduma hii muhimu inayopunguza magonjwa kama kipindu pindu,kuendesha na magonjwa mengine ya kuambukizana kutokana na uchafu na mbali na hivyo matumizi ya choo yanaleta faragha na stara kwani ukosefu wa choo ni jambo la kudhalilisha.


Shirika la Caritas Marsabit,imeanda sherehe hii ilikuwapa mafunzo kwa wakaazi wa eneo hilo kuhusu umuhimu wa kutumia vyoo.